Kesi ya rais wa migodi ya Pangea,North Mara yapigwa kalenda

07Dec 2018
Hellen Mwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kesi ya rais wa migodi ya Pangea,North Mara yapigwa kalenda

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imepiga kalenda kesi inayomkabili aliyekuwa rais wa Migodi ya Pangea, North Mara, exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika na wenzake mpaka Desemba 21,mwaka huu itakapotajwa.

Jana kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mfawidhi,  Huruma Shaidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika aliomba tarehe ya kutajwa.

Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa alidai kuwa mara ya mwisho kesi hiyo ilipotajwa, Jamhuri ulidai kwamba bado  kuna baadhi ya vielelezo wanavifanyia Kazi.

Kishenyi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo ni mpana kwamba kuna nyaraka zinafanyiwa kazi.

Hakimu Mhina alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 21, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu.

Mbali na Mwanyika washtakiwa wengine ni Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo,  Mkurugenzi mtendaji wa Pongea, North Mara na Bulyanhuku Assa Mwaipopo,kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza  Oktoba 17,mwaka huu.

 Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya USD  112 milioni.

Habari Kubwa