Kesi ya ubunge Njombe yapigwa tena kalenda

26Feb 2016
Furaha Eliab
Njombe
Nipashe
Kesi ya ubunge Njombe yapigwa tena kalenda

KESI ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Njombe Kusini inayomkabili mbunge wa jimbo hilo, Edward Mwalongo, imeahirishwa tena.

Mbunge wa jimbo Njombe, Edward Mwalongo.

Hatua hiyo imetokana na Wakili wa Serikali Apimark Mabrouk, kuweka mapingamizi mawili baada ya kuleta majibu yaliyoombwa na wakili wa mshitakiwa siku ya kwanza wakati kesi hiyo inatajwa.

Wakili wa upande wa mashitaka kupitia anaye msimamia Emmanuel Masonga ambaye amefungua kesi hiyo mahakama kuu kanda ya Iringa, Enos Swale, mahakama kuu inaiendeshea mkoani Njombe mbele ya jaji Jacob Mwambegele.

Mbele ya Jaji Mwabegele wakili wa serukali, Apimark Mabrouk aliweka mapinga mizi mawili baada ya kuleta majibu yaliyoombwa na wakili wa mshitakiwa siku ya kwanza wakati kesi hiyo inatajwa.

Mapingamizi hayo ni pamoja na kuwa maombi yaliyotolewa na wakili wa mlalamikaji, Enos Swale, ni kinyume cha kinyume na sheria za uchaguzi. Kutokana na mapingamizi hayo, Jaji Jacob Mwambegele wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, anayesikiliza kesi hiyo, aliahirisha kesi hiyo hadi Jumanne ijayo.

Katika kesi hiyo, Emmanuel Masonga wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anaiomba mahakama kutengua matokeo yaliyompa Mwalongo ushindi.

Walalamikiwa wengine katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Hilmar Danda, ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi.

Kesi hiyo inamkabili mbunge Edward Mwalongo, Mgurugenzi wa mji wa Njombe na Mwanasheria wa mkoa wa Njombe Hilmar Danda ambaye alikuwa ni msimamizi wa uchaguzi.

Habari Kubwa