Kibaha kupanda miti 10,000 miaka 60 ya uhuru

04Dec 2021
Julieth Mkireri
KIBAHA
Nipashe
Kibaha kupanda miti 10,000 miaka 60 ya uhuru

HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha inatarajia kupanda zaidi ya miti 10,000 katika maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru.

Miti hiyo inatarajiwa kupandwa katika maeneo mbalimbali kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi 

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Afisa Tarafa wa Kibaha Anatori Mhango wakati wa kupanda miti katika shule ya Sekondari Picha ya ndege amesema miti katika maadhimisho ya uhuru wamejipanga kutunza Mazingira kwa kupanda miti..

Anatori ametoa wito kwa shule nyingine kutumia mvua zilizoanza kunyesha kupanda miti kwenye maeneo yako kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi .

Afisa misitu wa Halmashauri ya mji wa Kibaha William Daud amesema katika  wameanza kupanda miti 200 katika shule hiyo na mingine itaendelea kupandwa katika maeneo mbalimbali.

Aidha William amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 wanatarajia kupanda miti zaidi ya laki 5.4 ambayo itapandwa kipindi cha masika

Mwalimu wa Mazingira wa shule ya Sekondari Picha ya ndege Richard Ndunguru amesema hadi sasa wamepanda miti 1000 katika shule yao ikiwemo ya matunda na kivuli. 

Habari Kubwa