Kidato cha Sita kuanza mitihani Juni 29

22May 2020
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Kidato cha Sita kuanza mitihani Juni 29

WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,  imetangaza mitihani ya kidato cha sita nchini itaanza Juni, 29 na kukamilika Julai 16, mwaka huu.

Waziri wa elimu, Prof. Joyce Ndalichako, picha mtandao

Akizungumza leo na Waziri wa elimu, Prof. Joyce Ndalichako, amesema wanafunzi ambao ni wa bweni wanatakiwa kuanza kuripoti Mei 30, mwaka huu ili ifikapo Juni mosi waanze masomo.

Ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kusambaza mitihani hiyo mara moja, lakini pia kuhakikikisha matokeo yanatoka kabla ya Agosti 30, mwaka huu.

"Tunataka  wanafunzi watakaofanya vizuri wapate muda wa kutuma maombi vyuo vikuu bila kuathiriwa na muda," amesema.

Kuhusu,  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Vyuo Vikuu amesema tayari bodi hiyo ina fedha kiasi cha Sh.Bilioni 122.8 kwa ajili ya wanafunzi wenye sifa ya kupata mikopo hiyo.

"Kinachotakiwa ni vyuo kuwasilisha nyaraka muhimu na hadi Mei 28, mwaka huu nyaraka hizo ziwe zimewasilishwa Bodi ya Mikopo ili itoe fedha hizo mara tu wanafunzi wanapofika vyuoni," amesema.

Habari Kubwa