Kigogo CHADEMA ajiuzulu Mbeya

15Jan 2019
Nebart Msokwa
Mbeya
Nipashe
Kigogo CHADEMA ajiuzulu Mbeya

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mbeya Mjini, Raphael Mwaitege, ametangaza kujivua wadhifa huo pamoja na nafasi zote alizokuwa anazishikilia ndani ya chama hicho pamoja na kujivua uanachama akidai kuwa anataka kupumzika siasa.

Akizungumza na wandishi wa Habari jijini hapa leo, Mwaitege amesema ameamua kuachana na chama hicho kikuu cha upinzani kutokana na vitisho alivyokuwa anavipata kutoka kwa wanachama wenzake waliokuwa wanamtishia maisha.

Hata hivyo ameweka wazi kuwa, pamoja na kutaka kupumzika siasa ili kunusuru maisha yake, anavutiwa na sera za Chama cha Mapinduzi (CCM).

Habari Kubwa