Kigoma yazindua mpango wa dharura mapambano vifo vya uzazi

20Apr 2021
Pendo Thomas
KIGOMA
Nipashe
Kigoma yazindua mpango wa dharura mapambano vifo vya uzazi

MKOA wa Kigoma umezindua mpango wa dharura wa kukabiliana na vifo vitokanavyo na uzazi baada ya vifo hivyo kuongezeka kwa miaka mitatu mfululizo na kufanya kuwa mkoa wa tatu kwa mikoa yenye vifo vingi vinavyosababishwa na uzazi  nchini Tanzania.

Akizungumza leo wakati wa uzinduzi wa mpango wa dharura wa kupunguza vifo vitokanavyo na wazazi na vifo vya watoto wachanga, mratibu wa afya  ya uzazi na mtoto Mkoa wa Kigoma, amesema mpango huo ni wa mwaka 2021 hadi 2023 na ukijikita kuboresha maeneo matano muhimu.

Maeneo ambayo mpango huo utayaangazia ni kuongeza idadi ya watoa huduma za afya ngazi ya jamii wakati wakiendelea kusubiri serikali kuongeza watumishi wa afya,kuongeza idadi ya wanawake wanao jifungulia klinik,kupunguza vifo vya watoto wachanga ,wajawazito na kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango.

Teyumwete ameeleza katika kukabiliana na jambo hilo kuna haja ya elimu ya uzazi salama kutolewa zaidi hasa kwa vijana wenye umri mdogo kwani katika vifo vya wanawake wajane.

Habari Kubwa