Kigwangalla akuta magogo 938 yaliyokaa miaka 10 bandarini

03Dec 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Kigwangalla akuta magogo 938 yaliyokaa miaka 10 bandarini

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla, ameagiza Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii atangaze kujitokeza kwa wamiliki wa magogo 938 yaliyokaa bandarini kwa zaidi ya miaka 10. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla akikagua kontena lililokuwa na magogo hayo bandarini.

Kama wamiliki wasipojitokeza, magogo hayo yatakuwa mali ya Serikali Kigwangalla ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandari ya Dar es salaam kufuatia uwepo wa taarifa za uvunaji holela wa magogo nchini, ambapo kuna taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wa kigeni wanagawa vifaa vya kuvunia bure kwa ahadi ya kuuziwa mzigo na wahusika.

Aidha taarifa zingine zilizosababisha ziara hiyo kufanyika ni kuwepo kwa taarifa kuwa kuna baadhi ya watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wanatoa vibali na kugonga nembo magogo hayo kinyume cha taratibu za kisheria. 

Mbali na hayo Dkt Kigwangalla ametoa siku 30 kwa wamiliki wa makontena 55 yanayodaiwa kuingizwa nchini kutoka Zambia kujitokeza na kuwasilisha nyaraka zao zenye kuthibitisha kama kweli yalivunwa nchini Zambia au la.

 

Habari Kubwa