Kigwangalla ataka bodi TANAPA kupunguza migogoro wananchi na hifadhi

08Feb 2020
Cynthia Mwilolezi
ARUSHA
Nipashe
Kigwangalla ataka bodi TANAPA kupunguza migogoro wananchi na hifadhi

WAZIRI wa Maliasili na Utalii  Hamisi Kigwangalla  leo amezindua Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) na kuiagiza kuweka misingi ya kutatua changamoto za kupunguza migogoro baina ya wananchi na hifadhi.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Hamisi Kigwangalla leo akikagua gwaride.

Agizo hilo alitoa leo jijini Arusha wakati wa uzinduzi huo ulioenda sambamba na kuwapatia vitendea kazi.

Alisema  baada ya Rais John Magufuli kuwaongezea muda wao mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuridhika na utendaji kazi wao, aliwaomba kuonheza kasi ya kushughulika na wahalifu  likamilifu na kukomesha matumizi ya silaha.

"Lakini sasa tangu muanzishe mfumo mpya wa Jeshi Usu naamini sasa mna uwezo wa kukamata wahalifu,kuwapekua na kuwafikisha katika vyombo vya sheria jambo ambalo awali halikuwepo,"alisema.

Aidha aliiagiza bodi kuchukua jukumu la kubaini kwanini licha ya kuwa na hifadhi 22 nchini lakini nyingi bado ni tegemezi.

"Naomba mtafute majibu ili tufike wakati vivutio hivi vinavyopatikana katika maeneo mbalimbali nchini vionekane kiuhalisia katika mapato ya nchi kiuchumi,"alisema.

Waziri wa Maliasili na Utalii,  Hamisi  Kigwangalla leo akikabidhi vifaa vya kazi baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) baada ya kuongezewa muda mwaka jana mwishoni na Rais John Magufuli.(Picha Na Cynthia Mwilolezi, ARUSHA)

Pia aliwataka kuweka mipango mbalimbali ya kuboresha miundombinu ili kuvutia watalii wengi zaidi katika hifadhi,sambamba na kuwekeza katika huduma bora za  malazi ikiwa ni pamoja na hoteli za kisasa.

Naye Kamishna wa Uhifadhi Dk.Allan Kijazi ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo alishukuru Rais John Magufuli kuwaongezea muda na kuahidi kuongeza nguvu ya kulinda rasilimali nchini.

"Lakini pamoja na haya yote kwa sasa tunakabiliwa na changamoto ya kupua kwa watalii kunakotokana na miundombini ya hifadhi kuwa mibovu sababu ya mvua zinazoendelea na mlipuko wa Virusi vya Korona,lakini tunaoambana kurekebisha niundombinu yetu,"alisema.

Dk.Kijazi pia alisema wapo mbioni kutekeleza maagizo ya Rais Magufuli ya kuanzisha kikosi cha ujenzi kama ilivyo kwenye vikosi vingine na tayari maandalizi yake yamefanyika na Machi mwaka huu wataanza rasmi kwa kushirukiana na majeshi mengine.

Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Jenerali Mstaafu George Waitara alisema alishukuru Rais Magufuli kuwaamini na kuridhika na utendaji kazi wao na kuahidi kutomwangusha katika kulinda rasilimalinza Taifa.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ni Kamishna Marijani kutoka Jeshi la Polisi,Prof.Wineaster Anderson kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk.Ruth Lugwisha toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC),Dk.Chanasa Ngeleja kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Wengine ni George Fumbuka Mshauri na Mtaalamu wa masuala ya Fedha,Devota Mdachi (Mkurugenzi  Mwendeshaji qa Bodi ya Utalii Tanzania TTB),Dk.Maurus Msuha (Mkurugenzi  Idara ya Wanyamapori,Dk.Allan Kijazi  (Katibu wa Bodi) na Jenerali Mstaafu George Waitara (Mwenyekiti wa Bodi).

Habari Kubwa