Kijana aliyekaa siku 127 ICU atoka hospitalini

06Sep 2020
Mary Geofrey
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Kijana aliyekaa siku 127 ICU atoka hospitalini

KIJANA Daudi Mikidadi (17) aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa siku 490, akisumbuliwa na tatizo la mapafu, ameruhusiwa baada ya hali yake kuimarika.

Daudi Mikidadi kushoto akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuruhusiwa kurudi nyumbani, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa MNH, Aminiel Aligaesha.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa MNH, Aminiel Aligaesha, amewaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuwa, kijana huyo baada ya kupokelewa Muhimbili alikaa kwenye chumba cha Uangalizi Maalum (ICU) kwa siku 127.

"Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga) imemruhusu Mikidadi kutoka hospitalini kwenda anakoishi na ataendelea kutumia mashine maalumu ya kumsaidia kupumua (Oxygen Concentrator), baada ya hali yake kuimarika," amesema Aligaesha. 

Ameeleza kuwa, baada ya kumpokea uchunguzi ulifanyika na kugundua kuwa mapafu yote mawili yameharibika kutokana na kuugua ugonjwa mmoja wapo wa mapafu (umehifadhiwa). 

Amesema kutokana na ugonjwa huo atahitaji usaidizi wa mashine ya kupumulia kwa maisha yake yote au kupandikizwa mapafu yote mawili.

"Watalamu wameridhika kwamba kwa hali aliyonayo sasa, anaweza kurudi kwenye kituo chake na Hospitali ya Muhimbili ikiendelea kushirikiana na kituo hicho kumpatia huduma za matibabu," amesema Aligaesha.

Habari Kubwa