Kikundi cha Isanjabadugu kilichovamia mashamba chapatiwa ufumbuzi

18Apr 2021
Richard Makore
Mbogwe
Nipashe Jumapili
Kikundi cha Isanjabadugu kilichovamia mashamba chapatiwa ufumbuzi

​​​​​​​KIKUNDI cha vijana kinachojiita Isanjabadugu kimevamia mashamba ya wakulima yenye ukubwa wa hekta 60 katika kijiji cha Nyakafuru wilayani Mbogwe mkoani Geita na kuanzisha uchimbaji wa madini ya dhahabu bila ya kuwa na leseni.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel.

Mkuu wa Wilaya Mbogwe mkoani Geita, Martha John, amekiri vijana hao kuvamia eneo hilo tangu mwaka 2017 na kuwatimua wakulima hao.

Kutokana na sakata hilo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel aliunda kamati ya kuchunguza suala hilo kwa agizo la Hayati John Magufuli na sasa imemaliza kazi yake na muda wowote ripoti itatolewa kwa jamii na  kwa Waziri wa Madini, Dotto Biteko.

Habari Kubwa