Kikwete ateuliwa kuwa Mwenyekiti Bodi ya GPE

30May 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Kikwete ateuliwa kuwa Mwenyekiti Bodi ya GPE

BODI ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), imemkaribisha Rais Mstaafu wa Tanzania awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete, kuwa Mwenyekiti mteule wa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Shule ya Uchumi na Sayansi ya Siasa ya London, huku Makamu Mwenyekiti mteule-

Dk. Jakaya Kikwete.

-akiwa ni Dk. Susan Liautaud.

Dk. Kikwete na Makamu wake wanatarajia kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu yao ifikapo Septemba 15, Mwaka huu.

Uthibitisho wa Dk. Kikwete umeonyesha umuhimu ambao GPE inaweka juu ya uongozi wa nchi washirika na ushiriki.Katika kipindi chote cha utumishi wa Dk Kikwete, katika serikali ya Tanzania na mashirika ya kimataifa na ya kikanda, alijitolea kuendeleza sera zinazoendelea za elimu na afya ya wanawake na watoto.

Mwenyekiti wa Bodi ya GPE na Waziri Mkuu wa zamani wa Australia Julia Gillard amewakaribisha viongozi hao wawili na kueleza namna alivyofurahishwa na uteuzi wao.

"Nimefurahi kuwakaribisha Dk. Jakaya Kikwete na Dk. Susan Liautaud sote tunafahamu kuwa Dk. Kikwete ni kiongozi anayeheshimika juu ya elimu na afya ya umma barani Afrika na kwingineko, ambaye uzoefu na taaluma yake ya utumishi wa umma itasimamia kazi ya GPE katika miaka ijayo lakini pia ustadi mkubwa wa Dk. Liautaud katika utawala na maadili utaimarisha mfano wa ushirikiano wa GPE kwa faida ya mamilioni ya watoto ulimwenguni. " amesema Gillard.

Kwa upande wake Dk. Kikwete amesema, “Ninaamini hakuna mabadiliko makubwa zaidi ambayo kiongozi anaweza kufanya ili kutumikia watoto walio katika mazingira magumu na waliotengwa zaidi ya elimu. Nimeheshimiwa kuongoza Bodi ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Elimu, shirika ambalo linajishughulisha na kushughulikia shida ya kujifunza ambayo imezidishwa na janga la corona," amesema Kikwete.

Habari Kubwa