Kilio wasafirishaji  wanyamapori hai

12Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Kilio wasafirishaji  wanyamapori hai

CHAMA cha Wasafirishaji Wanyamapori Hai Tanzania (Twea), kimeiomba Serikali kuifungulia biashara hiyo kwa kuwa wao hawakuhusika katika kusafirisha wanyama nje ya nchi.

Makamu Mwenyekiti wa Twea, Fatuma Hamisi.

Ombi hilo limetolewa baada ya Marchi 17 mwaka  2016 aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe, kuzuia biashara ya kusafirisha viumbepori nje ya nchi kufuatia kukamata ngedere Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) waliokuwa wakisafirishwa bila vibali.

Prof. Maghembe alisema alisitisha biashara hiyo ili kufanya tathmini ya viumbepori hai waliopo na kuwasaidia wafanyabiashara kupata bei stahiki.

Akitoa ombi la kufunguliwa kwa biashara hiyo juzi mjini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Twea, Fatuma Hamisi, kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga katika kikao cha kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya usafishaji viumbepori hai.

Hamisi alisema zuio hilo liliwakuta wakiwa na viumbepori hai,  hivyo wengi wamefariki kutokana na ukomo wa maisha yao huku wengine  wakifa kutokana na kukosa chakula.

“Kilio chetu hapa tunakuomba tufunguliwe ili tuendelee na biashara zetu kwani maisha kwetu yamekuwa magumu, tuna mikopo na tunasomesha na hapa Dodoma tumekuja kwa kukopa fedha,” alisema.

Hasunga alisema hawawezi kukubali ajira zizidi kupotea, hivyo maoni yao ameyapokea na atakutana na watendaji wa Wizara ili kuyatatua.

 

Habari Kubwa