Kiluwa adai Waziri Lukuvi alimkaba na kumpora mkoba wenye fedha

17Dec 2018
Hellen Mwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kiluwa adai Waziri Lukuvi alimkaba na kumpora mkoba wenye fedha

MFANYABIASHARA  Mohammed Kiluwa (50) ameiambia Mahakama ya Wilaya ya Ilala,  kwamba Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi alimkaba na kumpora mkoba uliokuwa na fedha zake. 

Kiluwa anakabiliwa na mashtaka ya  kutoa rushwa yaDola za Marekani 40,000 (sawa na  Sh. Milioni 90) kwa Waziri Lukuvi ili asiwasilishe hati ya umiliki wa kiwanja kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Kiluwa ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kiluwa Steal Group. Co.ltd na Kiluwa Free Processing Zone alitoa ushahidi wa utetezi wake leo mbele ya Hakimu Mkazi, Samweli Obas.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi,  Imani Madega kutoa utetezi wake, Kiluwa alidai kuwa Julia 14,mwaka huu  alipata taarifa kutoka kwa  Shabani Selemani kwamba anatakiwa kupeleka hati zake za viwanja ofisini kwa Waziri Lukuvi,  ndipo Julia 16, 2018 alifanikiwa kufika ofisini hapo kwa Waziri.

Alidai kuwa alitii wito huo alikwenda ofisini na alimkuta waziri huyo akiwa peke yake.

Shahidi huyo wa kwanza wa utetezi,  alidai kuwa alimkaribisha na baada ya kumuelekeza mahali pa kukaa alimuuliza hati zake ziko wapi, alimjibu ziko kwa mmiliki mwenza  ambaye kwa wakati huo alikuwa amesafiri.

Habari Kubwa