Kimboye aitaka UVCCM kujibu mapigo kwa wanatukana viongozi

06Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Mara
Nipashe Jumapili
Kimboye aitaka UVCCM kujibu mapigo kwa wanatukana viongozi

​​​​​​​MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Emmanuel Kimboye, ameutaka umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) mkoani humo kujibu mapigo ya watu wanaowatukana viongozi wa chama na serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan na Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.

​​​​​​​Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Emmanuel Kimboye.

Kimboye amesema hayo katika kongamano la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) la kumpongeza Rais Samia lililoambatana na kuchangia damu katika Hospitali ya Wilaya ya Butiama na kutembelea makumbusho ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Aidha, Mwenyekiti huyo akautaka umoja huo kuacha tabia ya kushiriki kutukana viongozi wa serikali kwenye mitandao ya kijamii na badala yake wasimame kukijenga chama.

Habari Kubwa