Kingu atimiza ahadi ujenzi kanisa la KKKT Musimi

02Jun 2020
Dotto Lameck
Singida
Nipashe
Kingu atimiza ahadi ujenzi kanisa la KKKT Musimi

​​​​​​​MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ametoa msaada wa mifuko 30 saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Musimi iliyopo Kata ya Sepuka wilayani Ikungi.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu (wa tatu kushoto) akikabidhi saruji mifuko 30 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Musimi.

Akizungumza wakati akitoa msaada huo jana, Kingu amesema anatimiza ahadi aliyoahidi baada ya kuombwa kusaidia ujenzi wa kanisa hilo.

“Mapema mwaka huu uongozi wa kanisa hilo uliniomba nisaidie mifuko 100 ya saruji kwa aliji ya ujenzi wa kanisa hilo ambapo leo hii nimetoa mifuko 30 ili kuendelea na ufyatuaji wa matofari” amesema Kingu.

Kingu amesema kuwa ahadi hiyo ataitoa kwa awamu tatu ambapo ameanza na mifuko hiyo 30 ili kazi iweze kuendelea na baadae atamalizia iliyobaki.

Pamoja na hayo, Kingu amekagua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kinyampembee na kuzungumza na wajumbe wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo ili kujua nini kinahitajika ili kusukuma ujenzi huo.

Habari Kubwa