Kingu- "Ulinzi mkubwa wa JPM unatokana na kunyoosha nchi"

14Apr 2019
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Kingu- "Ulinzi mkubwa wa JPM unatokana na kunyoosha nchi"

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu(CCM), amesema ulinzi kwa Rais John Magufuli unatokana na mambo makubwa anayoyafanya ya kunyoosha nchi.

Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu.

Akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2019/20, Kingu amesema ameshangazwa na kauli ya kiongozi wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe kudai kuwa amekutana na msafara wa Rais lakini ameogopa kutokana na kusindikizwa na magari zaidi ya 80. Kingu amesema suala la ulinzi na usalama kwa Rais lazima liwe kubwa na kushauri ulinzi wa raia uongezwe maradufu.

“Hatuwezi kuacha kutokana na mambo makubwa anayofanya hivyo usalamawake haupo sawa.Suala la utawala bora hakuna mahali palipoandikwa kuwa chama fulani kifanye vurugu au kundi la watuf fulani”amesema.

Akizungumzia maendeleo ya jimbo lake, Kingu amesema Wakala wa barabara Mijini na Vijijini (Tarura) wamepeleka kiasi cha Sh. Bilioni 1.3 na kwasasa wana madaraja na vituo vya afya na kudai kuwa hayo ndo mambo ya utawala bora.

Habari Kubwa