Kirusi cha Omicron chagundulika Marekani

02Dec 2021
Carlos Banda
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kirusi cha Omicron chagundulika Marekani

Kesi ya kwanza ya kirusi kirusi kipya cha Omicron kimegunduliwa katika Jimbo la California nchini Marekani ikiwa ni siku kadhaa tangu Rais wa taifa hilo, Joe Biden kusema kuwa, kuzuka kwa kirusi hicho sio jambo la kuchukua hatua ya kujifungia (Lockdown) bali ni jambo la kutafakari kwa umakini.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kirusi cha Omicron kimetajwa kuwa na uwezo wa kuleta madhara zaidi duniani kote.

Kirusi cha Omicron kiligunduliwa nchini Afrika Kusini na kimeendelea kusambaa na kugundulika katika mataifa mbalimbali huku wanasayansi wakiendelea kuchunguza kusambaa kwa kirusi hicho, athari yake kwa wagonjwa waliothibitika kupatwa na kirusi hicho na kiwango ambacho chanjo zilizopo zinaweza kupambana na kirusi hicho. 

Mpaka sasa kirusi hicho kimetajwa kuenea katika mataifa mbalimbali huku mataifa yaliyoendelea yakiweka kizuizi kwa nchi ambazo zimegundulika kuwa na kirusi hicho.

Habari Kubwa