Kisena ashtakiwa kuisababishia UDART hasara ya Sh.bil 2.41

11Feb 2019
Hellen Mwango
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kisena ashtakiwa kuisababishia UDART hasara ya Sh.bil 2.41

MKURUGENZI wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (UDART), Robert Kisena(46) na wenzake watatu wamefikishwa mahakama wakikabiliwa na mashtaka 19, ikiwamo kutakatisha Sh.Milioni.603 na kuisababishia mradi huo hasara ya Sh.Bilion 2.41.

MKURUGENZI wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (UDART), Robert Kisena akiingia mahakamani.

Mbali ya Kisena, washitakiwa wengine ni Kulwa Kisena(33), Charles Newe(47) na Cheni Shi (32).

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao leo Februari 11, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili wa Serikali George Barasa, ester Martin, Moza Kasubi na Imani Imtumezizi.

Barasa alidai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka hayo ikiwamo moja la kuongoza uhalifu, kujenga kituo cha mafuta bila kibali, kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa, wizi wakiwa Wakurugenzi, utakatishaji fedha manne na manne ya kughushi, manne ya kutoa nyaraka za uongo, mawili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja la kuisababishia mamlaka hasara.

Katika shtaka la kwanza ilidaiwa kuwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 kwa mamlaka waliyokuwa nayo waliosababishia UDART hasara ya Sh.bilioni 2.41.

Katika shtaka jingine ilidaiwa kuwa mshtakiwa wa kwanza na wa nne, Kisena na Shi, wanadaiwa kati ya Mei 26, 2016 wakiwa benki ya  NMB tawi la Ilala, wakiwa Wakurugenzi wa Kampuni  Longway Engineering huku Kisena akiwa kama Mkurugenzi wa UDART walifanya muamala wa Sh.milioni 603 kupitia akaunti ya benki ya UDART kisha kuzihamishia fedha hizo  katika akaunti ya Longway na baada ya siku mbili, wakijuwa fedha ni zao la kughushi.

Habari Kubwa