Kitabu cha Nyerere kilichopotea chapatikana

29Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Kitabu cha Nyerere kilichopotea chapatikana

Waziri wa Katiba na Sheria ,Profesa Palamagamba Kabudi amesema Kitabu cha Rais wa Awamu ya Kwanza Mwl.Julius Nyerere kinachoitwa 'Uhuru wa Wanawake' kilicholkuwa kimepotea kimepatikana.

Akizungumza jana ,Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha 'Tanzania Gender Bench Book on Women's' Profesa Kabudi alisema Kitabu hicho kilichoandikwa na Nyerere akiwa masomoni Uganda kilipotea na baadae kupatikana na kuchapishwa mwaka 2013.

Alisema Kitabu hicho kilichopatikana wakati tayari Mwalimu Nyerere akiwa amefariki sasa kimechapishwa na Chuo Kikuu cha Makerere kilichopo nchini Uganda kwa lugha ya Kiingereza na kinaitwa 'Women are Eagles not Chickens'.

Habari Kubwa