Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema hayo wakati akihojiwa na Televisheni za Taifa (TBC), kwenye kipindi cha Tunatekeleza na kusema hakuna mgawo wa umeme nchini.
Amesema tatizo la kukatika kwa umeme linatokana na kufanyika kwa marekebisho ya mitambo iliyochakaa kwa kudumu takribani miaka 40, amesema marekebisho yanayofanywa ni kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na mitambo itakayowezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika wakati wote.
Amesema kuna upungufu wa umeme kutokana na ukarabati unaoendelea, na kwamba mafundi wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha hali inakuwa sawa kufikia Disemba 15, mwaka huu.