Kunchela arudisha fomu, atoa msimamo wasaliti wa chama

09Jul 2020
Neema Hussein
KATAVI
Nipashe
Kunchela arudisha fomu, atoa msimamo wasaliti wa chama

Aliyekuwa Mbunge wa Vitimaalum Kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Roda Kunchela amekua mtia nia wa kwanza kurudisha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea ubunge Mpanda Mjini kupitia chama hicho.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Kunchela amesema yeye kama Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Katavi hawawezi kukubali kuona wanachama wa chama hicho wakiumizwa kwa usaliti.

Amesema chama hicho kimejengwa kwa nguvu kwani wapo waliopoteza kazi kwa ajili ya chama hicho hivyo hawawezi kukubari kuona watu wachache wanakiharibu kwa usaliti.

"Natoa rai kwa wagombea mwaka huu hatuko tayari kuona watu wachache wanasaliti chama kama kuna madiwani wamenunuliwa bora watoke kwa usalama vinginevyo tukimjua mtu huyo tuko tayari kumpoteza,"amesema Kunchela.

Amesema alipokua Mbunge wa Vitimaalumu alisimamia upotevu wa baadhi ya pesa katika baraza la madiwani lililopita pia migogoro mbalimbali ya ardhi.

Hata hivyo alikishukuru chama hicho kwa kumpa ushirikiano ndani ya miaka mitano alipokua Mbunge Vitimaalumu bila ya kupata tatizo la aina yoyote.

Amesema miaka hiyo imempa ujasiri wa kuamua kutia nia ya kuingia kwenye kinyang'anyilo cha kugombea ubunge kwani tayari anazijua vizuri changamoto zinazo wakabili wananchi.

Katibu wa chama hicho mkoa wa Katavi, Almasi Ntije amesema wamejipanga vizuri kushiriki uchaguzi pia alisema mwaka huu wanataka kuendesha siasa za kistaarabu.

Habari Kubwa