Kunenge awatoa hofu wakazi Mafia kuharibuka kwa Tishari

25Jan 2022
Julieth Mkireri
PWANI
Nipashe
Kunenge awatoa hofu wakazi Mafia kuharibuka kwa Tishari

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amewatoa hofu wakazi Wilaya ya Mafia baada ya kuharibika Tishari jambo ambalo limesababisha kukosekana kwa usafiri wa majini kwa siku zaidi ya tatu.

Kunenge ametoa kauli hiyo jana baada ya kufanya ziara wilayani Mafia ambapo amesema tayari vifaa vimeingia na mafundi wapo kazini kwa ajili ya matengenezo na kwamba Tishari litaanza kufanyakazi hivi karibuni.Tishari ni sehemu ambayo Meli au Kivuko kinapofika upande wa pili wa bahari au ziwa kinasimama na abiria kutelemka kwenda nchi kavu lakini kutokana na mvua na upepo huo Tishari hiyo ilisombwa na upepo na hivyo abiria kukosa sehemu ya kutelemkia."Nimekuja nimeona Tishari imepata madhara lakini tayari tumewasiliana na wenzetu wa Bandari  ambao ndio wenye Tishari hili na bahati nzuri wameanza kuchukua jitihada ili kurudisha hali ya kawaida, alisema KunengeKunenge, alisema kama kazi hiyo itafanyika usiku na mchana haitachukua muda mrefu ,hivyo amewaomba wakazi wa Mafia na wale wa Nyamisati wanaotegemea usafiri huo kuwa na subira wakati Serikali ikiendelea kufanya kazi.

Habari Kubwa