Kupungua kwa uzalishaji Maji Mtambo wa Ruvu Chini

08Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Kupungua kwa uzalishaji Maji Mtambo wa Ruvu Chini

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar-es-salaam (DAWASA) inawataarifu wananchi na wakazi wa Bagamoyo hadi Kigamboni kuwa huduma ya majisafi itakosekana kwa saa 24 kuanzia tarehe 08/06/2021 asubuhi hadi 09/06/2021.

SababuMatengenezo ya bomba kuu la usambazaji maji 54” linalotokea katika matenki ya chuo kikuu Ardhi eneo la Victoria na  makumbusho baada ya kupasuka.

Maeneo yatakayoathirika ni Mji wa Bagamoyo, vijiji vya zinga, kerege, Mapinga, Bunju, Boko, Mivumoni, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke, Uwanja wa ndege, Tegeta, kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach, Mlalakuwa,Mwenge, Mikocheni, Msasani, sinza, kijitonyama, oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, katikati ya jiji (City center), Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, hospitali ya Rufaa Mhimbili, Kigamboni Navy na Ferry

DAWASA inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza. 

Tupigie kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 na 0735 202121 (whatsap tu)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Jamii- DAWASA

Habari Kubwa