Kwimba watakiwa kupanda miti kukabiliana na jangwa

17Jun 2021
Neema Emmanuel
Nipashe
Kwimba watakiwa kupanda miti kukabiliana na jangwa

KATIBU Tawala Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike awataka wananchi wa Kwimba kupanda miti ili kuondokana na hatari ya kukabiliwa na jagwa litakalochangia upoteaji wa uoto asili.

Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike.

Hayo yameyasema baada ya mapitio ya hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2019 hadi 2020 wilayani Kwimba mkoani hapa.

"Wilaya ya Kwimba ni moja ya wilaya iliyoathirika na ukataji miti, tunaelekea kuwa jangwa ni wakati wa kulidhibiti kwa kuhamasishana kupanda miti hasa kwenye maeneo ya shule, hospitali,ofisi za serikali ,nyumbani na kauli mbiu inaweza ikawa kabla ya kukata miti mtu ahakikishe anapanda miti, akikata mti mmoja anapanda minne," ameeleza Samike.

Aidha akizugumzia suala la ukusanyaji wa mapato, amesema matatizo mengi yanayozikumba halmashauri ni ukusanyaji wa mapato hivyo wawe wabunifu wa miradi mbalimbali ambayo wakisimamia  vizuri na kudhibiti upotevu wa  mapato yata kuwa mengi na maendeleo yataenda kwa kasi.

"Hapa nimeona wanalalamika fedha lakini wakiangalia kuna posi ambazo wanasema hawapeleki fedha benki ni ajabu kwa nini mnashindwa kufuatilia ata hivyo vitu vidogo lakini bado mnasema mnategemea chanzo kimoja cha mazao mimi siamini kama hapa Kwimba mnategemea mazao peke yake mna vyanzo vigi ambavyo bado hamjavigundua mkiamua mtakuwa na vyanzo vingi vitakavyowaletea mapato mengi," amesema Samike.

Habari Kubwa