Lissu aibua madai kuvuliwa ubunge

20Jan 2019
Mary Geofrey
DAR ES SALAAM
Nipashe Jumapili
Lissu aibua madai kuvuliwa ubunge

MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, amedai kuwa amepata taarifa kuhusu njama zinazosukwa ili kumvua ubunge.

MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.

Katika taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii jana, iliyothibitishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika, kuwa ni ya Lissu, ilieleza kuwa mkakati huo umeandaliwa na Bunge kutokana na kutokuhudhuria vikao kwa muda mrefu.

“Nimepata taarifa, kutoka kwa watu wawili tofauti, kwamba kuna mkakati unaandaliwa wa kunivua ubunge wa jimbo la Singida Mashariki. Yaani hoja ni kwamba sijamwandikia Katibu wa Bunge taarifa yoyote ya maandishi kuhusu kuumwa kwangu wala matibabu yangu kwamba sijahudhuria vikao vya Bunge tangu Septemba 7, 2017 hadi sasa,” alisema Lissu.

Hata hivyo, taarifa hiyo ya Lissu ilikanushwa na Katibu wa Bunge, Stephen Kigaigai, ambaye aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa hana taarifa wala hajui kuwapo kwa mkakati huo ulioelezwa na Lissu.

Kwenye waraka wake, Lissu alisema kuwa sababu za kushindwa kuwasilisha taarifa za maandishi kwa sababu alipelekwa Nairobi nchini Kenya akiwa mahututi, viongozi wote wa Bunge walikuwa na taarifa za tukio hilo.

Habari Kubwa