Lissu atoa salamu za Mwaka Mpya

03Jan 2021
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Lissu atoa salamu za Mwaka Mpya

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewasilisha rasmi malalamiko yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) iliyoko Uholanzi, kikidai kutotendewa haki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka jana.

Kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, chama hicho kimelazimika kukimbilia kwenye mahakama hiyo ya kimataifa kikidai kulikuwa na ukiukwaji wa misingi ya uchaguzi wakati wa mchakato wa uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Lissu aliyoiita salamu za Mwaka Mpya, tayari chama hicho kimepokea taarifa ya kupokewa kwa malalamiko yao yaliyowasilishwa Desemba 24 mwaka jana.

"Kufuatia kuchafuliwa kwa uchaguzi mkuu na matukio mbalimbali yaliyofanyika kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba, chama chetu kilitangaza kitawasilisha malalamiko yake ICC baada ya mawakili wetu kuandaa nyaraka zote zinazohitajika.

"Leo kama sehemu ya salamu zangu za Mwaka Mpya, ninapenda kuwataarifu kwamba tarehe 24 Desemba, Kampuni ya Mawakili ya Amsterdam and Patners wa London, Uingereza na Washington DC, Marekani, iliwasilisha malalamiko kuhusu makosa dhidi ya ubinadamu na dhidi ya CHADEMA kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu," Lissu alisema.

Kwa mujibu wa Lissu, ambaye ni kitaaluma ni mwanasheria, malalamiko hayo huenda yakachukua muda mrefu uchunguzi wake kufanyika, akidokeza kuwa huenda ikawa zaidi ya miaka mitano.

Aliwataka wanachama wa chama hicho kuwa watulivu kusubiri kukamilika kwa mchakato huo wa muda mrefu ambao amedai una matumaini ya kile alichokiita kufufua demokrasia ya kweli.

CHADEMA ilishinda jimbo moja katika Uchaguzi Mkuu huo, huku ikishika nafasi ya pili katika kinyang'anyiro cha kuisaka nafasi ya urais...soma zaidi kupitia https//epaper.ippmedia.com

Habari Kubwa