Lissu mgombea urais Bara, Mwalimu mgombea mwenza

04Aug 2020
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Lissu mgombea urais Bara, Mwalimu mgombea mwenza

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimependekeza jina la Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara Tundu Lissu, kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika mwezi Oktoba.

Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara Tundu Lissu.

Matokeo ya mapendekezo hayo yametangazwa jana Agosti 3, 2020, na Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika, baada ya Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho kumpitisha kwa kura 405, akifuatiwa na Lazaro Nyalandu 36 na wa tatu ni Dk. Mayrose Majinge aliyepata kura 1.

Aidha pia Wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho, wamempendekeza Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu, kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wa Zanzibar pia Wajumbe wa Baraza hilo wamempendekeza Said Issa Mohamed, kuwa mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar.

 

Habari Kubwa