Lugha ya mbunge wa CCM yamkwaza waziri

25Apr 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Lugha ya mbunge wa CCM yamkwaza waziri

LUGHA yenye ukakasi iliyotumi- wa bungeni jana na Mbunge wa Ulanga Mashariki, Goodluck Mlinga (CCM) ilimfanya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, alazimike kutotoa kauli ya serikali kuhusu madai ya kuwapo wa wahadhiri wanaowa- felisha wanafunzi vyuoni kwa sababu zao bi

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (Ole Nasha)

Mara tu baada ya kumalizika kwa kipindi cha ‘Maswali’ bungeni mjini hapa jana asubuhi, mbunge huyo aliomba mwongozo kwa Spika akiitaka serikali itoe kauli kuhusu kuwapo kwa wahadhiri wanaowafelisha wanafunzi maku- sudi baada ya kunyimwa penzi au fedha.

Mlinga aliomba Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuangalia wahadhiri wa vyuo vikuu ambao alidai wamekuwa wakiomba penzi kwa wanafunzi wa kike kama kig- ezo cha kuwafaulisha.

Pia alidai walimu hao wamekuwa na utaratibu mpaka wapewe fedha na wanafunzi ndipo wawafaulishe.

Katika kujenga hoja yake, Mlinga alieleza kuwa awali katika kujibu swali la Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga (Chadema), Naibu Waziri wa Elimu alijibu kwamba kuna wanafunzi wanaonewa kwa kukaririshwa madarasa, hasa kwe- nye shule zinazomilikiwa na watu binafsi.

Mlinga alisema ana taarifa kuwa ipo tabia ya kuwakaririsha madarasa wanafunzi kwa kuwaonea katika vyuo mbalimbali nchini.

“Na hasa dada zetu wa kike na katika vyuo vikuu na walimu wanajulikana kabisa kuwa huyu mwalimu ni dume la mbegu. Kwa hiyo, kama mwanafunzi hatoi, hawezi kufaulu na kuna walimu wao wanajulikana kabisa wanataka pesa,” Mlinga alisema.

“Naiomba wizara baada ya hii nguvu kuiongeza katika shule za sekondari sasa waelekeze katika vyuo vikuu hasa kwa wanafunzi wa kike ambao wanaonewa.”

Katika mwongozo wake kwa mbunge huyo, Spika Job Ndugai aliyekuwa anaongoza kikao cha jana, alimsimamisha Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia (Ole Nasha) ili alitolee ufafanuzi jambo hilo. “Mheshimiwa Ole Nasha umepokea hii maneno eeeh!” Spika Ndugai alisema.

Ole Nasha alisema na kusema: “Mheshimiwa Spika nimepokea, sema maneno aliyotumia Mheshimiwa Mlinga yalinifanya niwe nasikiliza ukakasi zaidi kuliko hoja yake.” Naibu waziri huyo alisema atakutana na mbunge huyo ili amsikilize kwa kina hoja yake ilikuwa ipi na alikuwa anataka kusema nini bungeni.

“Lakini nitamshauri vilevile mdogo wangu kwamba hili ni Bunge, siku nyingine aangalie lugha ambayo anatumia kwa sababu ameongea maneno ambayo si mazuri. Lakini hoja yake nitazun- gumza naye,” alisema Ole Nasha. 

Habari Kubwa