Lugola atengua makamanda wa polisi

16Jan 2019
Augusta Njoji
Dodoma
Nipashe
Lugola atengua makamanda wa polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, ametengua uteuzi wa makamanda wawili wa mikoa ya kipolisi Ilala (Salum Hamduni), na Temeke (Emmanuel Lukula), kwa kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa ya kupambana na rushwa ndani ya jeshi la polisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, picha mtandao

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametengua uteuzi wa makamanda wawili wa mikoa ya kipolisi Ilala (SalumHamduni), na Temeke (Emmanuel Lukula), kwa kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa ya kupambana na rushwa ndani ya jeshi la polisi.

Aidha, Lugola ametengua uteuzi wa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Ramadhan Ng'anzi kwa kumchukulia hatua askari mzalendo aliyetoa taarifa kuhusu magendo ya biashara ya bangi na mirungi mkoani humo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu ameagizwa kuunda tume itakayofanya kazi miezi mitatu kuchunguza vitendo na mianya ya rushwa kwa kikosi cha usalama barabarani.

Habari Kubwa