Lukuvi akabidhi gari Katavi kurahisisha utendaji kazi

02Jul 2020
Neema Hussein
Katavi
Nipashe
Lukuvi akabidhi gari Katavi kurahisisha utendaji kazi

WAZIRI wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi, ameikabidhi halmashauri ya manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, gari lenye thamani ya Milioni 150/- pamoja na vifaa vya upimaji wa ardhi Kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi wa sekta hiyo.

Lukuvi amekabidhi gari hilo Julai 1, 2020, maara baada ya kuzindua ofisi ya ardhi katika mkoa huo.

Amesema hadi kufikia mwishoni mwaka huu vijiji vyote katika mkoa huo viwe vimepimwa na kupatiwa hati za vijiji.

Hata hivyo, amesema watu elfu 15 waliopimiwa viwanja vyao na baadhi ya watumishi wa idara hiyo wapewe hati za umiliki wa viwanja.

Lukuvi amesema kutokana na kuanzishwa kwa ofisi za ardhi nchini kumesaidia kuondokana na migogoro mbalimbali ya ardhi katika halmashauri za wilaya.

Kwa upande wake, naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, Angeline Mabula, ametoa rai kwa wakazi wa mkoa huo kulipa kodi ya ardhi wanayomiliki ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.

Juma Homera, mkuu wa mkoa huo amesema migogoro 300 ya ardhi imetatuliwa kati 500 iliyokuwa ikiikabili idara hiyo.

Habari Kubwa