Maadhimisho wiki ya maziwa kufanyika Tanga

30May 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Maadhimisho wiki ya maziwa kufanyika Tanga

MSAJILI wa Bodi ya maziwa nchini, Dk. George Msalya, amesema maadhimisho ya wiki ya maziwa ambayo huadhimishwa Dunia kote kila ifikapo Juni Mosi kwa Mwaka huu Kitaifa yatafanyika jijini Tanga.

Dk. George Msalya.

Msalya amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea madhimisho ya wiki ya maziwa duniani amesema karibu bilioni 22 zimekua zikitumika kuagiza maziwa kutoka nje hali ambayo imepelekea kuliumiza soko la ndani.

Msalya amesema suala la unywaji wa maziwa kwa Watanzania bado linaonekana kutokuwa na hamasa licha ya serikali kutumia juhudi kubwa katika kuhamasisha juu ya matumizi ya maziwa.

“Bado uelewa ni mdogo mtu badala ya kunywa maziwa wanakwenda baa kunywa pombe wakati maziwa ni muhimu kuliko hiyo pombe” amesema Msalya.

Aidha, Dk.Msalya amewataka watanzania kuwa na uzalendo wa kutumia bidhaa za ndani za maziwa ili kuwainua wafugaji, wasindikaji na wachakataji wa bidhaa hiyo kwani zipo bidhaa nzuri za maziwa zinazotengenezwa nchini.

Msalya amesema Tanzania bado ina uzalishaji mdogo wa maziwa kwani inazalisha Lita bilioni 3.4 ambapo ukigawanya kwa idadi ya watanzania, kila mtu atakunywa wastani wa Lita 50 tu kwa mwaka.

Habari Kubwa