Maafisa mazingira watakiwa kusimamia sheria kudhibiti mifugo mjini

25Apr 2019
Happy Severine
BARIADI
Nipashe
Maafisa mazingira watakiwa kusimamia sheria kudhibiti mifugo mjini

Katibu cha chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Donald amewataka maafisa mazingira wa Halmashauri zote za Mkoa wa Simiyu kuhakikisha wanawachukulia hatua za kisheria  wale wanaoachia mifugo yao inazurura mitaani  ovyo.

katibu wa chama cha mapinduzi CCM Donald Magesa akiwaongoza vijana wa chama hicho(green guard ) katika zoezi labuhamasishaji wa kupanda miti uliofanyika katika eneo la wazi mtaa wa Kidinda mjini Bariadi.

Katibu huyo ameyasema hayo Leo wakati ya kampeni ya uhamasishaji wananchi juu ya upandaji miti katika maeneo yao,iliyofanywa na vijana waCCM ( green guard) mjini Bariadi.

Amesema kuwa maafisa mazingira wanatakiwa kusimamia na kuzitumia sheria zilizowekwa za kuzuia uzururaji mifugo ili kutunza mazingira yaliyopo.

Magesa ameongeza kuwa katika kampeni ya upandaji miti inayoongozwa na vijana wa CCM kwa kushirikiana na shirika la  The Foundation of Joseph at Former Europe AID la Tanzania litasaidia kutoa mafunzo ya msingi ya nadhalia ya uhifadhi wa mazingira,upandaji na mwongozo ya kisheria ili kusaidia janga la mabadiliko ya tabia Nchi.

Nae Maduhu Masunga  kijana wa green guard amesema kuwa hali ya ukataji miti inaongezeka kwa kasi na kama haitadhibitiwa inaweza kuendelea kuleta madhara kwa jamii kutokana na mabadiliko ya tabia hasi.

Habari Kubwa