Maalim Seif aangukia pua Mahakama Kuu

18Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Maalim Seif aangukia pua Mahakama Kuu

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imekubaliana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kumtambua Prof. Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa CUF.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu Machi 18, 2019 na Jaji Benhajj Masoud.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, unamaanisha kwamba Maalim Seif Sharrif Hamad, siyo Katibu Mkuu wa CUF kwa hatua ambazo upande wa Prof. Lipumba imeuchukua kwa kumchagua Khalifa Suleiman Khalifa kuwa Katibu Mkuu.

Hukumu ya kesi hiyo ilifunguliwa na Bodi ya wadhamini wa chama hicho, baadhi ya wajumbe wanaoumuunga mkono Maalim Seif, dhidi ya Prof. Lipumba na msajili wa vyama wakipinga uamuzi wa msajili kumtambua Prof. Lipumba kuwa bado ni mwenyekiti halali wa CUF.

Habari Kubwa