Maalim Seif asisitiza Vyama vya Upinzani kushirikiana

04Aug 2020
Enock Charles
Dar es Salaam
Nipashe
Maalim Seif asisitiza Vyama vya Upinzani kushirikiana

MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif amesisitiza umuhimu wa vyama vya upinzani kuungana kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu ni kupata nguvu ya pamoja katika uchaguzi huo.

MWENYEKITI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif :PICHA NA MTANDAO

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) uliofanyika Mlimani City, Jijini Dar es Salaam amesema kuwa ingawa mazungumzo hayo yamechelewa kufanyika lakini chama hicho kitapigania muungano hadi dakika ya mwisho kwa kuwa ndio njia pekee ya upinzani kuibuka na ushindi.

“Jana nilimsikia mwenyekiti wa chadema akisema kuwa wana mazungumzo na act nataka nidhibitishe ni kweli na sio kwamba vyama vingine tumevitenga tulidhani kwamba tunahitaji kuweka msingi madhubuti na vyama vyote makini” amesema Maalim

Kauli ya Mwenyekiti huyo wa ACT-Wazalendo imekuja siku moja baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya uchaguzi na kupata washindi wa kura za maoni kwa nafasi za Urais kwa pande zote mbili za Muungano huko ACT-Wazalendo ikitarajiwa kufanya hivyo siku ya kesho.

 

 

 

 

 

 

 

Habari Kubwa