Maalim Seif atimkia ACT Wazalendo

18Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Maalim Seif atimkia ACT Wazalendo

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif, pamoja na wanaomunga mkono upande wake ndani ya chama hicho wametangaza kujiunga na ACT Wazalendo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Mahakama Kuu kumtambua Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ndiye mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa, amesema kuwa ameamua kujiunga na chama hicho baada kuona kuwa ni sehemu ya kukihujumu chama cha CUF baada ya dola kuingilia mhimili wa mahakama.

"Mimi na wenzangu katika uongozi tumetafakiri kwa kina juu ya upi uwe mwelekeo wetu iwapo maamuzi ya kesi yangekwenda hivi yalivyokwenda tumeona njia sahihi ni kutafuta jukwa nyingine ya kuendeleza mapambano ya kisiasa tuliokuwa tukiyasimamia kupitia CUF, jukwaa tuliloamua kwa kuelekeza nguvu zetu zote ni Chama cha Alliance for Change and Transparency," amesema Seif.

Aidha Seif amewataka wanachama na viongozi ambao walikuwa wanamuunga mkono kipindi akiwa CUF, wasisite kujiunga naye katika jukwaa hilo jipya kwa ajili ya kuendeleza mapambano ambayo wamekuwa wakiyapigania.

Habari Kubwa