Mabasi zaidi yafungwa 'luku'

17Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Mabasi zaidi yafungwa 'luku'

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imeanza kuyafungia vifaa vya kudhibiti mwendo kasi mabasi yatokayo Moshi, Arusha kwenda Mwanza, Musoma na Kahama.

Hatua hii ya pili imekuja baada ya mabasi yatokayo Dar es Salaam kwenda Dodoma, Singida, Mwanza, Musoma na Kahama kufungiwa vifaa hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Afisa Mfawidhi Sumatra Mkoa wa Manyara, Nelson Mmari, alisema ili kuepuka ajali nyingi zinazotokea nchini, taasisi hiyo imeamua kutafuta muarobaini wa tatizo la ajali zinazoweza kuepukika.

Alisema kifaa hicho kinafuatilia mwenendo wa basi liwapo safarini.

“Kifaa maalum cha kufuatilia mwenendo wa gari ni kifaa kinachofungwa kwenye gari la abiria kwa ajili ya kuchukua taarifa za mwenendo wa gari husika na kuzituma wakati huo huo kwenye mfumo maalum wa kufuatilia mwenendo wa gari,” alisema.

 

Habari Kubwa