Mabeyo atua Njombe kufuatilia mwenendo mauaji ya watoto

11Feb 2019
Na Mwandishi Wetu
NJOMBE
Nipashe
Mabeyo atua Njombe kufuatilia mwenendo mauaji ya watoto

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo ametinga mkoani Njombe na kufanya mkutano wa ndani na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Njombe pamoja na vikosi maalumu vilivyopo mkoani humo kwa ajili ya kuchunguza matukio ya mauaji ya watoto.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo alivyowasili Njombe.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe Mabeyo amesema “vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana pamoja na jeshi, na mimi ndiye mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi hivyo ninaowajibu na si kwamba jeshi limeingia sasa, hapana hatujafikia hatua ya kuingiza jeshi,”

“Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana pamoja na jeshi. Na mimi ndiye mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi hivyo ninaowajibu na si kwamba jeshi limeingia sasa, hapana hatujafikia hatua ya kuingiza jeshi,” amesema Mabeyo.

Amewataka wananchi kutulia kwani vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya kazi yake vizuri kuhakikisha waliohusika wanabainika, akisisitiza kuwa sababu ya kutekeleza mauaji hayo zinafahamika na kwamba taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.

Hivi karibuni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Renatha Mzinga amesema watuhumiwa 30 wanashikiliwa kutokana na kuhusika kwao na utekaji na mauaji ya watoto hao. 

Habari Kubwa