Mabilioni ya malipo yafanyika nje ya bajeti - CAG

08Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Mabilioni ya malipo yafanyika nje ya bajeti - CAG

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, imebaini kuwa Bil. 29/- zilifanyika kama malipo nje na taratibu za bajeti kwa baadhi ya taasisi za serikali.

Akiwasilisha ripoti hiyo Jijini Dodoma leo Alhamisi Aprili 8, 2021 CAG, Kichere amesema kuwa fedha hizo zilitolewa bila ya rsisiti za kielektroniki.

''Katika ukaguzi mwaka huu nilibaini kuwa malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 29 yalifanyika nje ya bajeti. Baadhi ya taasisi zilizofanya malipo hayo ni TANROADS, TAWA, TARURA, TIA, UNESCO, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu'' - amesema Kichere.

Habari Kubwa