Machali aonya uhujumu miundombinu

20Jul 2021
Restuta Damian
BUKOBA
Nipashe
Machali aonya uhujumu miundombinu

WANANCHI Wilayani Bu­koba mkoani Kagera Wametakiwa kuacha vit­endo vya uhujumu wa miundombinu ya Shiri­ka la Umeme (TANESCO) wilayani humo kwa kuchoma nguzo na wizi wa nyanya na kusab­abisha hasara.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Moses Macha­li wakati akizungumza na vyombo vya haba­ri mjini humo, baada ya kupokea taarifa ya matukio ya kiuhar­ifu wa wizi na uhuju­mu wa miundombinu ya umeme wilayani humo

Machali alisema, vit­endo vya wizi na uch­omaji wa nyaya za um­eme husababisha hasa­ra kwa Shirika na Wa­nanchi ambao hufanya shughuli za uzalisha­ji wa kipato kwa ku­tegemea nishati hiyo.

Alisema kwa mujibu wa taarifa za Shirika hilo ni kwamba, Mae­neo yaliyofanyiwa hu­juma ya uchomaji wa nyaya kwa baadhi ya Kata zilizomo wilaya­ni humo ni Kemondo,I­zimbya,Katoma,na Nya­nga.

Habari Kubwa