Madaktari Arusha kikaangoni

01Nov 2017
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Madaktari Arusha kikaangoni

Waganga Wakuu katika wilaya zote za mkoani Arusha wamepewa barua za onyo na Katibu Tawala wa Mkoa huo Richerd Kwitega kutoka na kushindwa kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa maboresho ya huduma za afya katika maeneo yao.

Miongoni mwa mambo ambayo hawakuyatekeleza ni pamoja na kutambua viashiria vya magonjwa yanayosumbua wanawake ikiwemo saratani ya shingo ya kizazi na kudhibiti wajawazito kujifungulia majumbani.

Wakizungumzia changamoto hiyo baadhi ya watendaji wa sekta hiyo ngazi ya wilaya wakiwemo waganga wakuu wamesema uhaba wa vitendea kazi, wataalam na ugumu wa Jiografia ya maeneo wanayofanyia kazi ni miongoni mwa vikwazo katika utekelezaji wa majukumu yao.