Madaktari wapinga kuongezwa mshahara

08Mar 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Madaktari wapinga kuongezwa mshahara

Madaktari zaidi ya 500 nchini Kanada pamoja na wanafunzi 150 wanaosomea fani hiyo wameandika barua ya wazi kupinga hatua ya ya chama cha madaktari nchini humo kupanga kuwaongezea mshahara.

"Sisi, madaktari wa Quebec ambao tunaamini kuwa mfumo wa umma ndio wenye nguvu zaidi, tumeamua kupinga kuongezeka kwa mshahara wa hivi karibuni uliotoka kwa Chama cha Madaktari nchini ," barua hiyo inasema.

"Ongozeko hili ni la kushangaza sana kwani wauguzi wetu, makarani pamoja na watalaamu wengine wanakabiliwa na hali ngumu sana za kufanya kazi, wakati wagonjwa wetu wanaishi na ukosefu wa upatikanaji wa huduma zinazohitajika kwa sababu ya makato kadhaa kwa miaka ya hivi karibuni na uongozi wa nguvu katika Wizara wa Afya, "inasomeka barua hiyo 

Kanada ina mfumo wa afya ya umma kwa watu wote ambao hutoa chanjo ya jumla ya huduma za afya zinazotolewa kwa lazima, badala ya uwezo wa kulipa huduma hiyo.