Madalali watakiwa kusajiliwa kuondokana na utapeli

10Dec 2019
Dotto Lameck
Dar es Salaam
Nipashe
Madalali watakiwa kusajiliwa kuondokana na utapeli

MWENYEKITI wa Chama Cha Madalali Tanzania TACA, Phidel Katundu, amewataka madalali wote nchini kujitokeza kwa ajili ya kusajiliwa ili watambulike na kuondokana na utapeli unaoendelea kwa baadhi ya watu wanaojiita madalali.

Phidel Katundu

Katundu amesema hayo leo katika kikao alichofanya na wanahabari katika ofisi ya chama hicho Jijini Dar es Salaam, huku akisema kuwa wanampango wa kuwasajili madalali wote katika chama hicho na kuweka taratibu za kuwakagua leseni kila mwaka kwa kuwa leseni nyingine zitakuwa zimefika mwisho.

“Tunampango kila ifikapo mwezi Januari tunamkagua kila mwanachama kama anavibali vyote ikiwemo kulipa kodi serikalini ama leseni zinazomruhusu kuwa dalali na tukishajiridhiisha tunatoa cheti kwenye chama ili watambuane na muda mwingine kushirikiana” amesema Katundu.

Aidha Bw.Katundu ametaja changamoto kubwa ambayo inawakabili ni kuingiliwa na madalali ambao si rasmi yaani ambao wamekuwa matapeli na kupelekea kuchafua sifa za mwanachama wa TACA.Madalali watakiwa kusajiliwa kuondokana na utapeli

Habari Kubwa