Madereva 494 wakamatwa kwa ulevi wakiwa barabarani

15May 2022
Na Mwandishi Wetu
Geita
Nipashe Jumapili
Madereva 494 wakamatwa kwa ulevi wakiwa barabarani

JESHI la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limekamata madereva 494 wakiwa wamelewa na wengine wakiwa na viashiria vikubwa vya ulevi kwa kipindi cha Mwezi mmoja wa oparesheni iliyofanyika nchini kuanzia April hadi sasa ambapo lengo la oparesheni hiyo ikiwa ni kupunguza ajali za barabarani.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbrod Mutafungwa.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilbrod Mutafungwa, ametoa kauli hiyo akiwa Mkoani Geita ambapo amesema wamekuwa wakiwapima madereva mbalimbali wa mabasi na malori na kubaini hali hiyo huku wakifikishwa katika vyombo vya sheria.

"Ulevi sio mzuri ila unakuta Dereva anaendesha huku amelewa au ameamka nazo pombe, tukimpima tukikuta alcohol kubwa tunamchukulia hatua" amesema Mutafungwa.

Aidha, Mutafungwa amesema wamebaini pia kuwa baadhi ya magari huzidisha idadi ya abiria huku akitoa onyo kwa madereva wa bodaboda kupakia mishkaki.

Habari Kubwa