Mafundi umeme wawe na leseni za EWURA

20Jul 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Mafundi umeme wawe na leseni za EWURA

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo, amewashauri wananchi kuhakikisha wanatumia mafundi umeme wenye leseni za Mamlaka hiyo ili kujiepusha na madhara yanayoweza kutokea kwa kuunganishiwa na vishoka.

Titus Kaguo.

Kaguo ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akitoa mada ya majukumu ya EWURA, kwenye semina kwa Taasisi ya Maendeleo ya Viziwi Tanzania(TAWAVITA), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa EWURA, Mhandisi Godfrey Chibulunje.

Amewasihi washiriki 30 wa semina hiyo ambao ni mafundi wa umeme kuhakikisha wanakuwa na leseni kutoka EWURA ili kufanya kazi zao vizuri.

“Ndugu zangu kwa sasa hakikisha hamruhusu fundi kuwatandazia nyaya kwenye nyumba zenu kama hana leseni za EWURA, ninyi mliopo humu na mhamasishe na wenzenu kuwa na leseni ili kufanya kazi zenu kwa ufanisi na uhuru,”amesema.

Habari Kubwa