Mafunzo maalum kuhusu taaluma kwenye sekta ya habari yanahitajika

01May 2022
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe Jumapili
Mafunzo maalum kuhusu taaluma kwenye sekta ya habari yanahitajika

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Taarifa kwa Wananchi, Deus Kibamba amesema kuwa mafunzo maalum kuhusu taaluma kwenye sekta ya habari yanahitajika ili kuimarisha sekta hiyo kwani uandishi wa habari na demokrasia vinategemeana katika kupiga hatua.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa mdahalo wa Mapinduzi ya Sekta ya Habari tangu Uhuru ulioandaliwa na REPOA na Media Space kwa ufadhili wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

Alisema kuwa hali ya ukuaji wa vyombo vya habari na uhuru wa habari ulikuwepo ata kabla ya Uhuru, hivyo uimarishwaji wa demokrasia unahitajika ili kunusuru vyombo vya habari nchini, licha ya uwepo wa hali ya ukuajia wa vyombo hivyo ingawa kasi yake hairidhishi.

Kibamba alisema kuwa vyombo vya habari na mfumo umesonga mbele hivyo kupima ukuaji wake kupitia mazingira ni jambo la muhimu na kinachotakiwa ni kupima maendeleo na siyo wingi wa vyombo.

"Demokrasia ya nchi iliyoimarika vyombo vya habari vinazidi kushamili ,hapa nchini miaka mitano nyuma vyombo vya habari vilipoteza mwelekeo ata vile ambavyo havikufungwa walifunga uzalishaji wenyewe ,vingine vilifungiwa hivi karibuni vimefunguliwa lakini bado hawajaanza uzalishaji hivyo demokrasia inaposuasua lazima vyombo vya habari vipoteze mwelekeo" alisema Kibamba.

Naye Dk.Peter Mataba alisema kuwa midahalo kama hiyo ni muhimu katika kukuza na kurejesha tasnia ya habari na kutambua inakotoka na inakoelekea hivyo ushirikiano unahitajika katika kulikamilisha ilo.

Aidha Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tafiti za Uchumi na Kijamii ( REPOA) ambaye pia ni mtafiti kutoka Stephen Mwombela alishukuru ushirikiano unaotolewa na Ubalozi wa Marekani wa kusaidia vyombo vya habari nchini ambavyo ni muhimu katika ujenzi wa vyombo huru vya habari vitakavyo chochea ujenzi kwa Taifa la haki la kidemokrasia.

Alieleza kuwa waandishi wa habari wanaendelea kujengewa uwezo na maarifa kwa waandishi wa habari ili kuweza kufanya Kazi zao vizuri hivyo ameomba ushirikiano uendelee kuwepo ili kuijenga sekta hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kutoka Ubalozi wa Marekani Mike Pryor alieleza kuwa miaka 60 ya mahusianao baina ya Tanzania na Marekani yamewezesha kuwepo kwa mapindizi na uhuru wa sekta ya habari kutokana na namna ambayo nchi hiyo imevutiwa kuona kunakuwa na ustawi mkubwa wa vyombo vya habari hapa nchini.

Alieleza kuwa siku zote za mahusianao baina ya Marekani na Tanzania imekuwa mstari wa mbele kusaidia kupigania na kuendeleza jitihada za kuwaendeleza waandishi wa habari waliopo kazini ili waweze kumudu kufanya shughuli zao vizuri ili kuchochea maendeleo ya uchumi na ujenzi wa demokrasia katika Taifa.

" Marekani ipo mstari wa mbele kupigania uhuru wa habari kwani ndio msingi wa mambo yote mazuri katika ujenzi wa Taifa" alieleza Pryor. 

Habari Kubwa