Mafuriko yaathiri wakazi 800 Iringa

24Mar 2020
Na Mwandishi Wetu
IRINGA
Nipashe
Mafuriko yaathiri wakazi 800 Iringa

Wakati Serikali ikipambana kutokomeza ugongwa wa virusi vya Corona nchini, hali ya wananchi wa kitongoji cha Mbingama katika kijiji cha Isele Halmshauri ya Wilaya ya Iringa iko hatarini zaidi baada ya kaya 218 kukosa makazi ya kuishi kutokana na mafuriko.

MAFURIKO.

Zaidi ya  kaya 218 zenye wakazi zaidi ya 800 katika kijiji cha Isele hawana makazi baada ya  kitongoji chao kufunikwa na maji huku nyumba zao zikisombwa na maji.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Isele, pamoja na Diwani wa kata ya Mlenge, Msafiri wameiomba serikali kuwanusuru wananchi na adha hiyo inayowakumba hivi sasa.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amezungumzia juu ya madhara hayo na kuagiza Afisa Ardhi wa Wilaya kufika eneo hili kupima usawa wa ardhi pamoja na kugawanywa kwa maeneo ya ofisi za kijiji.

"Naagiza Afisa Ardhi kuja hapa kupima usawa kwa usawa wa kila kijiji, kugawanya eneo la ofisi za kijiji na ofisi za kujenga Kituo cha Afya na kuanzia leo ni marufuku mtu kujenga hovyuo hapa, pawe pakavu au pabichi", amesema Kasesela.

Kutokana na  changamoto hiyo wito umetolewa kwa wasamalia kujitolea vifaa mbalimbali ili kuwasitili wananchi hao kutokana na changamoto inayowakabili.

Chanzo: www.eatv

Habari Kubwa