Magufuli amtumbua bosi wa TISS Modestus Kipilimba

12Sep 2019
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Magufuli amtumbua bosi wa TISS Modestus Kipilimba

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua na kumuapisha Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa kuchukua nafasi ya Dk Modestus Kipilimba.

Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Septemba 12, 2019 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa uteuzi wake umeanza leo.

Kabla ya uteuzi huo, Diwani aliyeapishwa Ikulu, Dar es Salaam leo alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Akizungumza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amemtaka kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kuweka mbele maslahi ya Taifa. Taarifa hiyo inaeleza kuwa Kapilimba atapangiwa kazi nyingine.

Habari Kubwa