Magufuli aagiza makontena ya makinikia kupigwa bei

24Jan 2020
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Magufuli aagiza makontena ya makinikia kupigwa bei

Rais John Magufuli ameagiza makontena ya makinikia yaliyokamatwa yauzwe kwa wateja na faida iende kwenye kampuni mpya ya Twiga, inayomilikiwa na Serikali na kampuni ya madini ya Barrick.

Magufuli ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya serikali pamoja na kampuni ya Twiga, Ikulu jijini Dar es Salaam.

"Yale Makontena ambayo yako bandarini ambayo tuliyashika sasa mkatafute wabia mkayauze, kwa faida ya Kampuni ya Twiga," amesema Magufuli.

Mkurugenzi mtendaji mkuu wa kampuni ya Twiga Mark Bristow, amesema kuwa hatua ambayo Rais Magufuli ameanzisha ya kuingia ubia na kampuni hiyo ni jambo weledi tofauti na ambavyo watu wanafikiri kuwa serikali ina niaya kuwafukuza wawekezaji.

“Watu wengi walisema msimamo wako unafukuza wawekezaji, lakini safari uliyoianzisha imetufanya tuamini kwamba lazima pande zote mbili zinufaike, huo ndio weledi,” amesema Bristow.

Habari Kubwa