Magufuli ateua wengine kuongeza nguvu uchunguzi mchanga madini

10Apr 2017
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Magufuli ateua wengine kuongeza nguvu uchunguzi mchanga madini

RAIS Dkt. John Magufuli ameteua wajumbe wengine nane wa kamati maalum itakayofanya uchunguzi wa madini yaliyomo kwenye mchanga wenye madini ulio ndani ya makontena yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

RAIS Dkt. John Magufuli.

Kamati hiyo ya pili kuundwa na Rais Magufuli inajumuisha wachumi na wanasheria ambao wataungana na kamati ya kwanza iliyoundwa na wataalamu wa masuala ya jiolojia, kemikali na uchambuzi wa kisayansi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja wajumbe wa kamati hiyo kuwa ni;

Prof. Nehemiah Eliachim Osoro
Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara
Dkt. Oswald Joseph Mashindano
Bw. Gabriel Pascal Malata
Bw. Casmir Sumba Kyuki
Bi. Butamo Kasuka Philip
Bw. Usaje Benard Usubisye
Bw. Andrew Wilson Massawe

Wajumbe hao wataapishwa na Rais Magufuli kesho tarehe 11 Aprili, 2017 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hii ni kamati ya pili ya kulifuatilia suala hilo, ambayo imesheni wataalam wa masuala ya madini na miamba.

Habari Kubwa