Magufuli atumbua maafisa wa Polisi Wilaya ya Meru

06Jul 2020
Enock Charles
DAR ES SAALAM
Nipashe
Magufuli atumbua maafisa wa Polisi Wilaya ya Meru

RAIS John Magufuli aameagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini kutengua uteuzi wa maofisa wa polisi katika Wilaya ya Meru akiwemo Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo kwa kushindwa kuthibiti madawa ya kulevya katika wilaya hiyo.

rais john magufuli.

Akizungumza wakati wa kuapisha viongozi wapya aliowateua hivi karibuni Rais Magufuli ameagiza kutenguliwa kwa viongozi hao kufuatia Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya ,James Kaji kukamata madawa katika wilaya hiyo.

“Mnapita kwenye mji mnakuta magunia ya bangi mnaenda kwenye mji mwingine mnakuta magunia ya bamgi na madawa ya kulevya hii inaonyesha kuna kasoro kidogo kwa viongozi waliopo kule “ amesema Rais Magufuli

Akiongea na viongozi hao wateule Rais Magufuli amewataka kutimiza majukumu yao katika maeneo yao ili kuharakisha huduma kwa wananchi.

Habari Kubwa